Mwanaume mmoja Raia wa Zambia anayefahamika kwa jina la Mbewe ame-make headline kwa kuweza kuishi na wake zake wanne kwenye nyumba moja.
Kupitia Interview yake inayotrend huko Zambia aliyofanya na Mchungaji Jimmy Kay aliulizwa kwamba unawezaje kuwamiliki na kuwatunza wanawake wote?
Mbewe akajibu kwamba "Sitafichua ni nani aliyeniambia haya, lakini mmoja wao alisema mzee wewe ni mzuri, kucheat hakuna maana hasa kuwaridhisha licha ya umri mkubwa".
Aidha wake zake wawili kati ya wanne wamesema wanaridhishwa na Mbewe ni mwanaume wa kweli na hakuna mwanaume mwenye mwanamke mmoja hata akikununulia Mercedes Benz au Mjengo wa kuishi.