Dar es Salaam. Mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari Mpigimagohe iliyopo Mbezi, Abdul Kasuku (16) amejiua kwa kujinyonga kwa waya huku sababu za kujinyonga kwake zikiwa hazijafahamika.
Kamanda wa Polisi Kinondoni, Ramadhani Kingai amekiri kupokea taarifa hizo na kueleza kwamba amewatuma askari kwenda eneo hilo kwa uchunguzi zaidi.
"Nikweli nimepokea hizo taarifa lakini kuna askari wameenda kufanya uchunguzi kubaini chanzo kilichopelekea tukio hilo,"amesema Kingai
Akielezea tukio hilo baba wa moto huyo, Yahya Kasuku ameeleza kuwa mwanaye alijinyonga leo Jumatano Machi 16, 2022 asubuhi kwenye shamba lilipo jirani na nyumbani kwao huku yeye akiwa amepumzika ndani.
Amesema kuwa kabla ya kutokea kwa tukio hilo alishangaa kuona mwanaye hajaenda shule kama ilivyo kawaida yake licha ya kwamba alishapewa fedha kwa ajili ya matumizi ya shule pamoja na mdogo wake.
"Nilimuuliza mbona hujaenda shule akanijibu nitaenda lakini baadaye mama yake aliniambia alikuwa anatapika,"
"Hata hivyo nilimkazia lazima aende shule nikiamini kutapika pekee hakuwezi kumfanya ashindwe kwenda shule," amesema Kasuku
Ameeleza kuwa baada ya kumuelekeza mwanaye, aliendelea kupumzika akiamini kwamba atafanya hivyo, akiwa amepumzika ghafla mke wake alikuja kumuamsha na kumueleza mwanaye amejinyonga.
"Baada ya kutoka kuja pale kweli alikuwa amejinyonga kwa kutumia waya aliofunga kwenye tawi la mti wa mwembe akiwa bado anaangaika nikamshika miguuni na kumuambia mke wangu akate kamba lakini hata hivyo hatukufanikiwa kuokoa maisha yake," amesema
Kwa upande Mjumbe wa Mbezi Sukusi Kusini, Shomary Sengo ameeleza kuwa baada ya kupokea taarifa hizo alifika kwenye tukio hilo na kujiridhisha kabla ya kutoa taarifa Polisi