Mhitimu wa kike katika Chuo Kikuu cha Zambia (UNZA), Grace Matafwali(29) jumapili juzi akitoa ushuhuda katika kanisa la Gospel Mission lililopo Lusaka nchini Zambia amesema alichukua uamuzi huo baada ya kujiunga chuoni hapo miaka minne iliyopita kisha kulazimishwa kufanya ngono na baadhi ya wahadhiri hao na kupata maambukizi ya VVU.
Grace amesema wanafunzi wa kike kulazimishwa kufanya ngono chuoni hapo ni kitendo kinachofanywa na wahadhiri wengi.
Pia amesema kwa kuwa alikuwa yatima, alikosa mahitaji muhimu hali iliyomlazimu kukubali kwa shingo upande kufanya ngono na wahadhiri watatu tofauti waliomtaka kimapenzi kwani ukikataa wanakufelisha mitihani makusudi
Hakujua kati ya hao wahadhiri watatu ni yupi hasa alimwambukiza virusi lakini baada ya muda kupita alianza kupata dalili zisizo za kawaida na alipoenda akakutwa ameathirika
Grace amsema hali ya kukutwa na maambukizi ilimvuruga na kumfadhaisha sana akili sababu alilazimishwa na yeye alikubali kuepuka kufelishwa mitihani na wahadhiri
Baadaye ndio akaamua kulipiza kisasi kuwaambukiza wahadhiri wengine wengi na amesema kila alipokutana nao kimwili alihakikisha sehemu zake ni kavu na anapata michubuko na ngono bila kinga ili mlengwa asitoke salama
Japokuwa yeye aliambukizwa makusudi, lakini amesema baadaye akaanza kujutia kuambukiza wengine ndio maana ameenda kanisani kuungama