Mwanamke auawa Igunga, mwili watupwa shambani




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao
Tabora.   Mkazi wa mtaa wa Kamando kata ya Igunga Mjini wilaya ya Igunga, Veronica Jackson Juma (26) ameuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa kwenye shamba la mahindi.

Mwili huo umekutwa umefungwa kamba kwenye mikono na mdomo kuzibwa na kipande cha nguo.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Machi 3, 2022 Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kamando, Celina Mitimingi amesema jana Jumatano.

Amesema kuwa mwili huo umekutwa ukiwa hauna nguo na ulichukuliwa na polisi kupelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga.


 
Baadhi ya majirani na ndugu wa mama huyo wameeleeza kuwa tangu juzi usiku hawakumuona nyumbani na waliamua kumpigia simu na kuzungumza naye lakini muda mfupi simu hiyo ilikata.

"Wakati tukiendelea kuzungumza naye muda mfupi simu yake ilikatwa ghafla na haikuweza kupatikana tena" amesema Magreth James ambaye ni ndugu wa marehemu.

Baba wa marehemu, Jackson Juma amesema alipigiwa simu na ndugu zake kujulishwa kuwa mwili wa mwanawe umekutwa shambani.


Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Dk Merchades Magongo ameeleza kuwa walipokea mwili huo asubuhi na wameuhifadhi wakisubiri kuufanyia uchunguzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao alipoulizwa juu ya tukio hilo amesema tukio hilo lipo huku akibainisha kuwa anasuburi taarifa kamili kutoka kwa Polisi Wilaya ya Igunga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad