Mwandishi wa Urusi aliyekatiza habari kupinga vita hajulikani aliko



Mwandishi wa habari wa Urusi ambaye alikatiza kkipindi cha moja kwa moja cha habari kweye televisheni kupinga vita vya Ukraine ameripotiwa kutoweka.

Marina Ovsyannikova, mhariri katika kituo cha Channel 1 inayodhibitiwa na serikali, alizuiliwa baada ya kukimbia kwenye seti siku ya Jumatatu akiwa ameshikilia bango la kupinga vita.

Ishara hiyo, iliyoonekana wazi kwa sekunde chache, iliandikwa: "Hakuna vita, komesheni, msiamini propaganda, wanawadanganya hapa."

Bi. Ovsyannikova hajulikani alipo.

Mawakili wa Bi Ovsyannikova wanasema wamekuwa wakimtafuta mteja wao lakini hawajampata.


 
Mmoja wao, Anastasia Kostanova, aliambia BBC Idhaa ya Kirusi kwamba amekuwa akijaribu kumtafuta Bi Ovsyannikova kwa njia ya simu lakini simu yake haikupokelewa.

Kitendo cha mhariri huyo kukatiza taarifa ya habari ya moja kwa moja kupinga vita ni sawa na "uhuni", msemaji wa Kremlin amesema.

"Msemaji wa Putin, Dmitry Peskov alinukuliwa na shirika la habari la Urusi Interfax akisema: "Kumhusu msichana huyu, huo ni uhuni."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad