Mdau wa muziki nchini na Mtangazaji wa Clouds Media, @mwijaku ameonekana kukitaka cheo cha usemaji wa shirikisho la Muziki nchini. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mwijaku ameweka wazi kuwa kama vigezo ni elimu,basi anayo na kama kigezo ni kuwa mdau wa muziki, ana uzoefu na muziki kupitia THT.
Hili limekuja baada ya hii leo Mbunge na msanii wa Hip Hop, @mwanafa kwenye kikao cha wasanii kudai vigezo kama elimu na uzoefu, @stevenyerere2 hana, hivyo hafai kuwa msemaji wa shirikisho hilo.
Unahisi hii nafasi inamfaa Mwijaku?