Jenerali Sergiy Knyazev akifuatialia msafara wa wanajeshi wa Urusi wanaoelekea Kiev katika kambi ya jeshi
Maelezo ya picha, Jenerali Sergiy Knyazev akifuatialia msafara wa wanajeshi wa Urusi wanaoelekea Kiev katika kambi ya jeshi
Katika katika chumba maalumu chao kupeana taarifa za vita, majenerali wawili wa Ukraine wanaohusika na kuilinda Kiev wanaiambia BBC jinsi vikosi vyao vinavopambana kwa bidii ili kuizuia Urusi kuingia katika mji huo na kuelezea kwa nini wanaamini mji mkuu huo wa Ukraine una ngome muhimu dhidi ya Warusi.
Kiev inaathirika zaidi na vita hiyo, pamoja na silaha za nguvu zenye uharibifu mkubwa za Urusi.
Lakini katikati ya Kiev na vitongoji vyake vingi bado havijaguswa na silaha za Urusi. Miji mingine ya Ukraine inashambuliwa kwa mabomu na kumekuwa na majeruhi wengi.
Raia waliobaki wa Kiev, labda nusu, wamehamia magharibi mwa Ukraine au kuondoka nchini humo. Lakini wanakabiliwa na uzoefu huo wa kikatili.
Mito na maeneo ya tepetepe yanavyosaidia ulinzi
Majenerali hao wanaohusika na ulinzi wa Kiev wanasema Ukraine inapambana kwa nguvu, lakini wanakiri kwamba mji mkuu huo uko katika hatari ya kushambuliwa na makombora.
Hata hivyo, eneo la juu la mji huo ni la aina yake, anasema Jenerali Andriy Kryschenko. Mji huu mkubwa umegawanywa na mito, sio tum to mkubwa unaoitwa Dnieper unaigawanya Kiev, lakini pia vijito vyake vinavyounganisha mto huo.
"Ni vigumu kuuulinda kote, ikizingatiwa kuwa ni mji mkubwa sana," anasema. "Lakini kwa upande mwingine, ni faida kwetu. Mito na madaraja yako kwenye milango ya mji. Wanajeshi wetu wanaweka ulinzi na ulinzi."
Mengi zaidi
"Karibu na mji kuna mito mingi midogo ambayo hutiririka kuingia mto Dnieper na kuna maeneo tepetepe mengi ya maji maji na tepetepe , ambayo inamaanisha kuwa eneo hilo halifai kwa harakati kubwa za kijeshi."
Jenerali Kryschenko, ambaye pia ni naibu meya, amekuwa akivaa mavazi ya kawaida ya kijeshi kama ambayo rais wake Volodymyr Zelensky amekuwa akivaa anapozungumza na watu wake, kuwavutia washirika wake na kuwakasirisha maadui zake.
Faida nyingine, kwa ujumla, ni kwamba Kiev ni mji wa viwanda, ambapo viwanda na karakana hizo zimekuwa sehemu muhimu ya kutengeneza ngome: mtofali ya saruji, mifuko ya mchanga na vikwazo mbalimbali vya kupambana na vifaru.
Jenerali Andriy Kryschenko (katikati) salisema kwamba eneo linalozunguka Kyiv inawafanya wanajeshi wengi wanaotaka kuingia katika mji huo kupata shida
Maelezo ya picha, Jenerali Andriy Kryschenko (katikati) salisema kwamba eneo linalozunguka Kyiv inawafanya wanajeshi wengi wanaotaka kuingia katika mji huo kupata shida
Kryschenko na Knyazev wanataza skrini kubwa wanayoitumia kufuatilia mienendo ya vikosi vya Urusi kuingia Kiev.
Wanaelezea kwamba walikuwa wameshambulia na kuzuia mashambulizi makubwa mawili: moja kutoka mashariki na moja kutoka kaskazini magharibi, ukiwemo msururu mkubwa wa magari ya kivita ya Urusi wa kilomita 64.
Madaraja ya kimkakati
Kaskazini magharibi mwa nchi hiyo bado kunalengwa zaidi na Urusi. Ni upande wa pili wa Mto Irpin, karibu kilomita 20 kutoka katikati ya Kiev.
Ukraine imepeleka vikosi vyake vilivyojipanga vizuri na vyenye silaha nzuri, ambavyo viliyabomoa madaraja ya kimkakati. Maelfu ya watu waliokimbia makazi yao kutoka mji wa Irpin wamekuwa wakivuka mtohuo kwa kupita juu ya mabaki ya daraja lililovunjwa, wakiwa na mbwa na paka wanaowamilikia.
Lakini Jenerali Knyazev anasema: "Hiii ni ardhi ya ajabu sana, na hawawezi kupitia. Kama kusingekuwa na wanajeshi wetu katika eneo hilo la mto , wangeshambulia daraja kirahisi. Lakini tuko pale na tunataka kuwaangamiza."
Alipokuwa akizungumza, kombora jingine lililipuka sio mbali na la kwanza. Sauti ya milipuko hiyo inaweza kusikika wazi katika chumba tulichojuwepo cha kupeana taarifa za kivita. "Sikiliza," alisema afisa mmoja mdogo, "hiyo ilikuwa silaha zetu za anga imeangusha ndege nyingine."
Lakini kombora hilo liliupiga mji huo. Dereva wa basi aliuawa wakati kombora hilo lilipotua na kusababisha mlipuko mkubwa ambao pia uliharibu majengo kadhaa.
Chanzo cha picha, Getty Images
Daraja lililoharibiwa mjini Irpin
Maelezo ya picha, Daraja lililoharibiwa mjini Irpin
Mafanikio ya kijeshi ya Ukraine yamewashangaza washirika na maadui zake. Rais na makamanda wake wanafurahishwa zaidi na utendaji wa jeshi lao na maelfu ya watu wa kujitolea.
Hata hivyo Warusi bado hawajaweka nguvu zao kamili katika mji huu mkuu