Nato Yalaumiwa kwa Mauaji ya Raia, Ukraine




Naibu waziri mkuu wa Ukraine amesema Nato inahusika kwa kiasi fulani na vifo vya raia nchini humo kwa kushindwa kuweka zuio la ndege kuruka nchini Ukraine.

Akizungumza na BBC Radio 4, Olha Stefanishyna alisema "ni unyama kujua kwamba idadi ya raia na watoto watauawa kwa kutochukua uamuzi huo".

"Damu za hawa raia - ikiwa ni pamoja na mama na baba wa watoto wawili ambao walizaliwa jana tu na leo tu wanapoteza wazazi wao kwa kupigwa makombora - lawama sio tu kwenye mikono ya Urusi."

Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine aliomba radhi kwa kutokuwa mwanadiplomasia katika chaguo lake la lugha, lakini alisema alikuwa akizungumza "akiwa ameketi kwenye makazi ya mabomu".


Wanachama wa Nato wamekataa kuanzisha eneo lisilo na ndege kwa vile wanahofia kuzidisha mzozo huo kwa kuweka vikosi vya Magharibi katika vita vya moja kwa moja na nguvu za anga za Urusi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad