Imetolewa Barua rasmi kutoka kwenye Uingozi wa FreeNation inayomilikiwa na Rapper @naytrueboytz inayobeba ujumbe wa Msanii @naytrueboytz kujiondoa katika Tuzo za Muziki wa Tanzania (TMA) kutokana na kutokuwa na imani na Kamati ambayo imesimamia mchongo wa ukamilifu wa upangaji wa categories za Tuzo hizo.
Barua inasomeka -“Uongozi wa Freenation Rec Label Leo Tarehe 24/03/2022 Inatangazaa Kujitoa Kwenye Tuzo Za Mziki Za Tanzania Music Award Hivyo Basi Msanii Emmanuel Elibarick (Nay Wa Mitego) Sio Mshiriki Wa Tuzo Hizo Uwamuzi Huu Umetokana na Uwongozi Wa Freenation Rec Label Kutokuwa na Imani na Kamati Ya Uchambuzi Wa Kazi(Academy) Hivyo Basi Tunaomba Radhi Mashabiki Na Wadau Wa Mziki Waliopenda kumuona Emmanuel Elibarick (Nay Wa Mitego) Kuendelea Kuwepo Kwenye Hizi Tuzo Hivyo Basi Mashabiki na Wadau Wa Mziki Tuomba Msitishe Kupiga Kura Kuanzia Sasa. Uwamuzi Huu Ni Kwa Jili Ya Kutete Haki Ya Kila Msanii Na Masilahi Ya Mziki Wetu Wa Tanzania.
Aidha Uongozi Wa Freenation Rec Label Unawataka Mashabiki Na Wadau Wote Kuendelea Kumuunga Mkono Mkurugenzi (Ceo) Wa Freenation Rec Label Emmanuel Elibarick(Nay Wa Mitego) Kwenye Kazi Yake Ya Mziki”
Mtazamo wako ni upi Shabiki na Mdau wa Maendeleo ya Sanaa ya Tanzania!? Tuandikie kwenye Uwanja wa comments.