Ndoa ya Mrema ni Kesho, Aeleza Atakavyoenda Kanisani



Siku moja kabla ya kufunga ndoa Mwenyekiti wa TLP Taifa, Dkt. Augustino Mrema amesema atajaribu kujikokota kuelekea Kanisani na kama itatokea ataishia njiani kutokana na afya yake kutokuwa sawa, anaamini Paroko atajua nini cha kufanya

Mrema amesisitiza kuwa huduma ya Kanisa inapatikana popote, ikitokea ameshindwa kwenda Kanisani anaweza kufungishwa ndoa chumbani kwake au hata kitandani ilimradi wahusika wameridhia

Ameongeza “Kuhusu jina la mke wangu mtarajiwa mtalijua siku ya ndoa, pia kutakuwa na sherehe nyumbani kwangu pamoja na ibada”

Ndoa hiyo inatarajiwa kufungwa Machi 24, 2022 katika Parokia ya Uwomboni, Kijijini kwake Kiraracha

#JamiiForums

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad