Neema amkana Mzee Mrema “Sina Mpango wa Kuolewa”



Mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Neema Swai anayedaiwa kuolewa na Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Mzee Lyatonga Mrema amemkana mzee huyo akisema hamjui wala hana mpango wa kuolewa.

Neema amesema hayo kupitia kipindi cha Clouds 360 kinachoruka kupitia Clods TV leo Machi 23, 2022 asubuhi kufuatia picha zake kusambaa mitandaoni huku akihusishwa kuolewa na mzee huyo.

“Simjui Mzee Mrema na sijawahi kukutana naye. Nilikuwa nimelala asubuhi naamka nakuta missed call nyingi. Kwenye WhatsApp nikatumiwa Screen shot kuwa naolewa na Mrema.

“Siolewi na Mzee Mrema, hizi habari zinazozushwa na picha yangu kusambaza mtandao kuwa naolewa naye ni uongo na uzushi. Picha inayosambaa ni yangu niliipost kwenye page yangu watu wakaichukua na kuiunganisha na ya Mzee Mrema na kuisambaza mtandaoni.


 
“Kwa sasa sina mpango wa kuolewa na mwanaume yoyote yule. Nikipata nafasi ya kuongea na Mzee Mrema nitamwambia amwonyeshe mke wake hadharani ili ijulikane kuwa sio mimi ndiye Bibi Harusi. Siku ya jana sikwenda chuo kwa sababu wanafunzi wenzangu walikuwa wakinitania,” amesema Neema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad