Hadi sasa katika nyimbo zake Harmonize bado anamzungumzia Diamond, iwe moja kwa moja au kwa kuzunguka, ni kama anatapika nyongo kimtindo. Hizi ni ngoma tano za Bosi huyo wa Konde Music ambazo kampitia Diamond;
🍁UNO
Huu ulikuwa ni wimbo wake kwanza kuutoa tangu aachane na WCB, ulifanya vizuri sana, huku Harmonize alimrusha Diamond pamoja na mzazi mwenziye, Zari The Bosslady.
"Uno la Chibu Chibu linamkondesha Zari" aliimba Harmonize wimbo huo licha ya wawili hao kuwa tayari wameachana na Diamond alikuwa na mahusiano na Tanasha Donna toka nchini Kenya.
🍁KUSHOTO KULIA
Katika ngoma hii Harmonize anamshukuru Diamond kama miongoni mwa watu waliomleta mjini na kumpa nafasi, na kutaka choko choko zisiingizwe katika muziki wao.
"Peace kwa walionileta mjini Mondi wa Tandale, maneno majungu tupa chini muziki utawale" aliimba Konde Boy ambaye katika video anaonekana kama mtumwa aliyeruhiwa ambaye amevunja minyororo na kuondoka zake.
🍁USHAMBA
Ukiachana na wimbo wenyewe, pia video yake iliibua gumzo kufuatia Harmonize kumtumia kijana mwenye kufanana na Diamond kwa asilimia kubwa.
"Halina meno hilo Simba Zee, likila demu lazima litangaze", inajulikana na Diamond ndiye amekuwa akitumia jina la Simba katika muziki, ukiachanganya na yule kijana anayefanana naye katika video, ikatoa picha kamili kijembe hicho kinaenda kwa nani hasa.
Hadi sasa katika nyimbo zake Harmonize bado anamzungumzia Diamond, iwe moja kwa moja au kwa kuzunguka, ni kama anatapika nyongo kimtindo. Ebu endelea nayo.
🍁USIA
Hii ni ngoma mpya inayopatikana kwenye albamu yake mpya 'High School' ambayo ilitoka mwishoni mwaka jana, huku napo kampitia Diamond vilivyo, utakumbuka ngoma mbili za awali zipo katika albamu yake, Afro East.
"Simba na ukali wake wote ila akimuona Tembo anachimba, ila hiyo haimfanyi Tembo kuvimba" anaimba Harmonize ambaye amekuwa akitumia jina la Tembo katika muziki wake, huku akijichora na tattoo ya mnyama huyo mwenye nguvu za kutosha.
🍁WAPO
Kufuatia tukio la Mama mzazi wa Diamond, Bi. Sandra maarufu kama Mama Dangote kudai kuwa Mzee Abdul Juma Issack si baba halisi wa Diamond bali ni baba mlezi, Harmonize hakulikalia kimya hilo, akatoa ngoma; Wapo.
"Mama na Baba ndio nguzo ya dunia watunze wote , sio wakiume analia lia bila msaada wowote" aliimba Harmonize
Mwisho....... ✍