P -Square na Mpango wa Kuweka Historia 02 Arena "Tunaenda Kuifunga 02 Arena"


Nyota wa muziki nchini Nigeria ambaye anaunda kundi la P-Square, Peter Okoye, ameweka wazi kuwa P-Square wanauwezo wakufanya matamasha bila kuachia kazi mpya na yakafanya vizuri matasha hayo.

Haya yanajiri baada ya wakali hao kuwakata mashabiki kuchagua kati ya ukumbi wa O2 Arena ama Wembley (uwanja wa taifa wa Uingereza) waende wakafanye show yao. Maoni ya mashabiki wengi yameuchagua 02 Arena unaoingiza takribani watu elfu 20. Chaguo hilo ni kutokana na mfuatano wa wasanii nchini Nigeria kufanya show zao hapo na kutaka kuwashindanisha na wakongwe hao.

"Hatuhitaji kuujaza O2 Arena, tunaenda KUUFUNGA kabisa, iwe tumeachia kazi mpya ama hatuna kazi mpya. Mkongwe ni mkongwe" - amesema Peter Okoye akiwajibu mashabiki ambao wana wasiwasi endapo watashindwa kuujaza ukumbi huo.

Una mtazamo gani, Je P-Square wataweza kuujaza O2 Arena⁉️

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad