Pambano la Kiduku, Kabangu utamu kolea



MABONDIA wa ngumi za kulipwa Twaha Kiduku na Alex Kabangu, leo wamepima uzito tayari kwa pambano la kuwania mkanda wa ubingwa uzani wa kati unaotambuliwa na Shirikisho la Masumbwi la UBO Afrika.

Mabondia hao wamepima uzito nje ya eneo la Kituo Kikuu cha mabasi cha Msamvu, Morogoro na kuhudhuriwa na mashabiki, ambapo kila mmoja alitamba kuibuka mbabe.

Pambano hilo litapigwa kwenye ukumbi wa Tanzanite uliopo Morogoro mjini na litakuwa la raundi nane.

Mara baada ya kupima uzito, Kiduku aliwawahakikishia Watanzania kuwa atafanya vizuri kwa kumchapa mpinzani wake.


 
"Nimejiandaa vizuri kwa ajili ya pambano la kesho Jumamosi, naamini nitashinda, kwa sababu nitakuwa nacheza kwenye mkoa wangu, ambao kipindi kirefu sijacheza, niwaambie nitashinda bila wasiwasi kutokana na maandalizi niliyofanya, kikubwa tumuombe Mungu tuamke salama," amesema Kiduku.

Kwa upande wa Kabangu raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), alisema yeye amekuja nchini kwa kazi moja ya kuhakikisha anashinda pambano bila ya kuangalia kama itakuwa kwa pointi au kwa KO, lakini anachokiangalia zaidi ni kushinda pambano lake.

"Nadhani kesho wadau wa ngumi wasubirie kuona pambano zuri, niwashukuru mashabiki ambao wamejitokeza hapa kwenye uzito na kesho waje kwa wingi kuangalia pambano, " amesema Kabangu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad