Muda mfupi baada ya Wakili wa Mfanyabiashara, Ghalib Said Mohamed (GSM), Alex Mgongolwa kuweka wazi juu ya vielelezo vya umiliki wa eneo la kiwanja namba 60 lililopo Regent Estate Kinondoni, Dar es Salaam, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda ametoa kauli dhidi ya #GSM
Makonda amenukuliwa akisema “GSM usinilazimishe kusema uozo wako, achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua”
Wakili Mgongolwa ameeleza kuwa vielelezo walivyonavyo ni kutoka Wizara ya Ardhi vinavyompa uhalali mteja wake GSM kuwa Mmiliki. Kumekuwa na taarifa kuwa #Makonda naye anadai eneo hilo ni mali yake