Anatoly Chubais amejiuzulu kutoka jukumu lake kama mjumbe wa kimataifa na kutoroka Urusi
Duru ilidokeza kuwa Chubais alijizulu na kuondoka Urusi kutokana na vita vya Ukraine
Kujiuzulu kwake ni baada ya Rais Putin kuonya kwamba ataisafisha Urusi dhidi ya "uchafu na wasaliti" anaowatuhumu kufanya kazi kisiri na Marekani
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amepata pigo kubwa baada ya mmoja wa washauri wake, Anatoly Chubais kujiuzulu kutoka jukumu lake kama mjumbe wa kimataifa.
Pigo Kubwa kwa Rais Putin Baada ya Mshauri wake Kujizulu na Kutoroka Urusi
Anatoly Chubais kujiuzulu kutoka jukumu lake kama mjumbe wa kimataifa. Picha: Andrey Rudakov/Bloomberg.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini Urusi, Chubais kwa sasa yuko Uturuki na mke wake.
Chubais, 66, ambaye ni mwanamageuzi mkongwe wa Urusi, alipewa kazi ya kuratibu malengo ya maendeleo endelevu ya taifa hilo kimataifa.
Kujiuzulu kwake kunakujia baada ya kuchapisha picha ya kiongozi wa upinzani wa Urusi, Boris Nemtsov aliyeuawa mnamo Februari 2015, katika kile kilichoonekana kama ishara mbaya wakati vita vya Urusi na Ukraine vilipoanza.
Hata hivyo, hakuambtanisha ujumbe wowote katika kumbukumbu ya kuuawa kwake Nemtsov akionyesha kupinga uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Natazamia Kuona Tiketi ya Ruto - Karua Itakayookoa Taifa la Kenya: Moses Kuria
Japo hajatoa taarifa yoyote kuhusu kujiuzulu kwake, duru ilidokezea shirika la habari la Reuters kuwa Chubais alijizulu na kuondoka Urusi kutokana na vita vya Ukraine.
Akijulikana kama mbunifu wa ubinafsishaji wa Urusi wa miaka ya 1990, Chubais alimpa Putin kazi yake ya kwanza Kremlin katikati ya miaka ya 1990, na aliunga mkono kupanda kwake mamlakani mwishoni mwa muongo huo.
Chini ya Putin, Chubais alichukua nyadhifa za juu katika makampuni makubwa ya serikali hadi rais huyo alipomteua mjumbe maalum mwaka 2021.
Kujiuzulu kwake pia kunakujia baada ya Rais Putin kuonya mnamo Machi 16, 2022, kwamba ataisafisha Urusi dhidi ya "uchafu na wasaliti" anaowatuhumu kufanya kazi kwa siri na Marekani.
"Watu wowote, na haswa watu wa Urusi, wataweza kila wakati kutofautisha wazalendo kutoka kwa takataka na wasaliti na kuwachomoa kama kisu aliyeruka vinywani mwao kwa bahati mbaya."
"Nina hakika kwamba utakaso huu wa asili na muhimu wa jamii utaimarisha tu nchi yetu, mshikamano wetu, mshikamano na utayari wa kukabiliana na changamoto yoyote," Rais Putin alisema.
Ngilu Ataka DP Ruto Kukoma Kujipiga Kifua Kisa Kumsaidia Uhuru Kupata Urais: "Ni Uhuru Alikupa Ajira"
Wiki iliyopita, Arkady Dvorkovich, ambaye alikuwa mshauri mkuu wa uchumi wa Dmitry Medvedev wakati wa urais wake na naibu waziri mkuu hadi 2018, alijiuzulu kama mkuu wa hazina ya teknolojia ya Skolkovo inayoungwa mkono na serikali baada ya kulaani uvamizi huo.
Dvorkovich, ambaye pia ni rais wa Shirikisho la Kimataifa la Chess, ni mmoja wa maafisa wachache waandamizi wa zamani waliozungumza dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.