Polisi Yamtaka Paul Makonda Afuate Sheria na Taratibu Madai ya Kutishiwa Risasi



KAMANDA wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema Jeshi la Polisi halijapokea malalamiko yoyote kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuhusu madai ya kutishwa kupigwa risasi.

Jana, kwenye mitandao ya kijamii kulisambazwa video fupi ikimwonyesha Makonda akilalamikia alichokiita kupokwa eneo mkoani Dar es Salaam huku kukiwa na madai kwamba ametishiwa kupigwa risasi.

Alipotafutwa na Nipashe kuzungumzia suala hilo, Kamanda Muliro alisisitiza kufuatwa kwa utaratibu uliowekwa kisheria kushughulikia jinai nchini.

"(Makonda) ametishiwa na nani? Mtu akitishiwa si anakwenda kituo cha polisi? Mwambie 'tupe namba ya kesi uliyoishtaki inayochunguzwa polisi'. Mashtaka hayafunguliwi kwenye mitandao," alisema.

Kamanda Muliro alisisitiza kuwa mashtaka yoyote yanayotakiwa kuchunguzwa na Jeshi la Polisi, hayafunguliwi kwenye mitandao ya kijamii bali kwenye vituo vya polisi.


"Vituo vya polisi vifungwe ili vibaki kwenye mitandao kama anavyoripoti kwenye mitandao?" Kamanda Muliro alihoji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad