Rais wa Urusi, Vladimir Putin amepiga marufuku Warusi kuhamisha fedha nje ya nchi, wakati akijaribu kuzuia kushuka kwa thamani ya fedha hizo, kufuatia kuwekwa kwa vikwazo.
Putin amepiga marufuku hiyo kuanzia leo Machi Mosi, 2022 kwa kuhamisha fedha hizo kwenye benki na taasisi nyingine za kifedha nje ya Urusi.
Katika taarifa yake kupitia tovuti ya Kremlin, Putin amesema uhamisho wa fedha bila kufungua akaunti ya benki kwa kutumia njia za elektroniki za malipo zinazotolewa na wauzaji wa kigeni wa huduma za malipo pia zitapigwa marufuku.