RAIS Joe Biden amesema kuwa Rais Vladimir Putin wa Urusi "alikosea vibaya" kuamuru uvamizi wa kijeshi katika nchi jirani ya Ukraine, akidai amejaribu "kutikisa misingi ya ulimwengu huru."
"Katika historia yetu tumejifunza somo hili - wakati madikteta hawalipi gharama kwa uchokozi wao, husababisha machafuko zaidi," Biden alisema katika ufunguzi wa hotuba yake Capitol Hill Jumanne usiku.
Biden alidai zaidi kwamba "Vita vya Putin vilipangwa na bila kuchochewa" kwani kiongozi wa Urusi "alikataa juhudi za kidiplomasia" na "alifikiria Magharibi na NATO haitajibu."