Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema Naibu wa Rais, William Ruto alikuwa akimuhujumu na kusimamia mipango ya kumfanyia hujuma ili ashitakiwe
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Kikuyu waliomtembelea Ikulu Jijini Nairobi, jana Machi 26, 2022 huku akisisitiza Raila Odinga ndiye mtu sahihi kwa Nafasi ya Urais wa Kenya katika uchaguzi wa mwaka huu
Kenyatta amesisitiza kuwa Ruto alikuwa na uchu wa madaraka, alifanya mipango ili Rais ang’oke kisha yeye achukue madaraka kwa mlango wa nyuma huku akidai kuwa alikuwa akipinga hata kitendo cha Kenyatta kupatana na Odinga
#JamiiForums #Kenya