Mzozo unaendelea baina ya Urusi na Ukraine unazidi kuibua hisia za watu wengi Dunia, akiwemo Rais Mstaafu wa Ukraine, Petro Poroshenko aliyeamua kushika Mtutu na kuingia mtaani.
Mbali ya kushika mtutu wa Bunduki, Rais huyo mstaafu aliyehudumu kipindi cha mwaka 2014 hadi 2019 ametoa maneno makali kwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin.
Kupitia video aliyorekodiwa na kusambaa katika mitandao na vyombo mbalimbali vya habari, Poroshenko anaonekana akiwa mtaani kashika bunduki huku nyuma yake kukiwa na kikundi la Wanajeshi.