Rais Samia "Polepole kabla hujaenda Malawi tutazungumza kwa kirefu"




Dodoma. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewapa maagizo viongozi wawili aliowaapisha leo Jumanne Machi 15, 2022.

Viongozi hao ni Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Waziri Kindamba.

Akizungumza baada ya kuwaapisha viongozi hao katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, Mkuu huyo wa nchi alianza na Balozi Polepole huku akisema kuwa atakutana naye wazungumze kwa kirefu.

“Mheshimiwa Balozi (Polepole) najua baada ya hapa watakuweka darasani kwanza pale Chuo cha Diplomasia utakapotoka pale kabla hujaenda Malawi nitakutana na wewe, kwa hiyo tutazungumza kwa kirefu” amesema Rais Samia kwa kifupi akimuelekeza Polepole ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa mbunge wa kuteuliwa.


Akimpa maagizo Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Rais Samia amemtaka kwenda kuangalia suala la lishe pamoja na kuhamasisha chanjo katika mkoa huo.

“Mkuu wa Mkoa (Waziri Kindamba) unakwenda Njombe, ni mkoa wenye kila kitu kwa hiyo kama utatulia unaweza ukapandisha kipato kwa kiasi kikubwa pale Njombe lakini kuna mambo mengi ya kuangalia, pamoja na kuwa Njombe ni mkoa unazalisha chakula kwa wingi sana lakini kuna tatizo la nutrition, kalitazame hilo,

“Huko nyuma nilifanya mikataba na wakuu wa mikoa, walifanya vizuri, nafikiria pia kufanya mikataba na wakuu wa mikoa kusimamia mambo ya nutrition” amesema Rais


Amemuagiza RC Kindamba kusimamia chanjo ya Uviko-19 akimtaka kuhamasisha wananchi kuchanja.

Rais awaapisha Polepole, Kindamba

Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Machi 15, 2022 amemuapisha Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi. Soma zaidi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad