"Kuna tetesi nyingi nazipata ndani ya Jeshi la Magereza, nalisema hapa kwasababu Maofisa na Maaskari wote mko hapa, inaelekea Jeshi la Magereza hamuongei lugha moja, wengine wanavuta Kusini wengine Kaskazini, nina taarifa kwamba mnachungana kwa mabaya kila Mtu anamchunga mwenzie akosee iwe ishu, niwatake mdumushe umoja na mshikamano, mkiendelea kuvuta huku na huku hamtofika mbali"
"Jeshi hili sio mali yenu ni mali ya Watanzania, tumewaamini tu kuwapeni mtoe huduma kwenye Jeshi, yoyote atakayekuwa tayari kurudisha nyuma kwa ajili ya nafsi yake nasi tutakwenda nae pamoja, mkishikana mtakwenda haraka zaidi"
"Hampendani hamna umoja naomba rekebisheni, nendeni pamoja ili mfanye makubwa zaidi"———Rais Samia akizindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya Makao Makuu ya Magereza, Dodoma leo