Rais Vladimir Putin nguli wa upelelezi anavyoendelea kuisumbua Marekani



Marekani. Putin ambaye ni gwiji la upelelezi katika taasisi ya KGB, aliingia madarakani Desemba 31, 1999 wakati ulimwengu ulikuwa kwenye hofu kubwa ya kompyuta kutofanya kazi kuelekea mwaka 2000.

Licha ya Muungano wa Soviet (USSR) kusambaratika mwaka 1991, Putin ameonekana kuja na aina mpya ya utawala unaorejesha nguvu ya Russia, kwani kwa miaka 20 sasa, kiongozi huyo amegeuka kuwa kirusi kinachoisumbua Marekani na mataifa ya Ulaya Magharibi.

Bila shaka Putin ni adui mkubwa zaidi, mgumu kushughulika naye kuliko hata Leonid Brezhnev au Nikita Khrushchev, Waziri Mkuu wa Usovieti wakati wa mgogoro wa kombora la Cuba.

Kiongozi huyo ndiye mpangaji mkuu wa migogoro mingi kutoka Chechnya hadi Crimea, kutoka Syria hadi jiji kuu la Salisbury.


 
Ameonyesha kuwa na ushawishi hata kubadili uamuzi wa Umoja wa Mataifa mara kadhaa na kutokana na ushawishi huo, amefanikiwa kuidhoofisha Marekani.

Putin aliingia madarakani wakati wa hali mbaya ya Magharibi, ambapo Marekani ilikuwa nchi pekee yenye uwezo mkubwa kiuchumi.

Marais kadhaa wa Marekani wamejikuta wakifuata mitazamo ya Putin. Kwa mfano, Bill Clinton aliyeingia madarakani karibu sawa na kiongozi huyo aliwasilisha malalamiko ya usumbufu wa Putin akitaka kupanuliwa kwa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi (Nato) hadi katika mipaka ya Urusi.


Kwa upande wake, Rais George Bush aliyeingia baada ya Clinton, aliwahi kueleza kutomwelewa Putin.

“Nilimwangalia mwanamume huyo machoni. Nilimwona moja kama mtu mwaminifu na niliweza kupata hisia ya nafsi yake,” aliwahi kusema Bush katika tamko lake maarufu wakati walipokutana mara ya kwanza huko Slovenia mwaka 2001.

Bush alifikiri kimakosa kwamba angeweza kuanzisha chuki dhidi ya Putin na kumshawishi kwa upole kurejea katika njia ya kidemokrasia.

Japo Bush alitembelea Urusi zaidi ya nchi nyingine yoyote, ikiwa ni pamoja na ziara mbili za kibinafsi chumbani kwa Putin huko St Petersburg, kiongozi huyo wa Urusi tayari alikuwa akionyesha mienendo hatari ya kidhalimu.


 
Mwaka 2008 ambao Bush alimaliza kipindi chake madarakani, Putin aliivamia Georgia katika kile Russia ilichokiita ni operesheni ya utekelezaji wa amani.

Wakati Marekani ikihoji sababu ya uvamizi huo, Russia nayo ilihoji sababu ya Marekani kuivamia Iraq.

Alipoingia madarakani Barack Obama alijitahidi kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Russia. Waziri wake wa kwanza wa mambo ya nje, Hillary Clinton alifanya kazi kwa karibu na mwenzake wa Russia, Sergey Lavrov ambaye mpaka sasa anashikilia wadhifa huo.

Hata hivyo, Putin alijua Marekani baada ya vita vyake vya muda mrefu huko Afghanistan na Iraqi, haitakuwa na mamlaka ya kulinyooshea kidole Taifa lingine kwa sababu na lenyewe linafanya uvamizi.


Mwaka 2013 wakati Obama alipokataa kutekeleza onyo lake dhidi ya Bashar al-Assad baada ya kiongozi huyo wa Syria kutumia silaha za kemikali dhidi ya watu wake, Putin alichukua fursa hiyo kwa kumuunga mkono Assad kutekeleza vita vya mauaji na kuimarisha ushawishi wa Moscow Mashariki ya kati wakati Marekani ilikuwa inataka kujiondoa katika eneo hilo.

Mwaka uliofuata alinyakua jimbo la Crimea, na kujikita katika eneo la mashariki mwa Ukraine, licha ya kuambiwa na Obama kujiondoa, Putin hakusikia.

Kama hiyo haitoshi, Putin alitaka kushawishi matokeo ya uchaguzi wa urais wa Marekani 2016 kwa matumaini kwamba Hillary Clinton, adui wa muda mrefu, angeshindwa na Donald Trump, shabiki wa muda mrefu, kijana mpenda anasa angeshinda.

Tajiri huyo wa mali New York hakuficha kueleza jinsi anavyomvutia Putin, mbinu ya kujipendekeza ambayo ilimvutia zaidi Putin.

Russia ilifurahia sana wakati Trump alipoikosoa hadharani Nato, akadhoofisha mfumo wa muungano wa Marekani baada ya vita.


 
Rais huyo anayeisumbua Marekani akawa mchonganishi kiasi kwamba aliiacha Marekani ikiwa imegawanyika zaidi kisiasa kuliko wakati wowote, tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kiongozi wa Marekani anayetajwa kwa kumudu mpambano na Russia ni George Herbert Walker Bush, aliyetawala Marekani miaka 30 iliyopita tangu kuanguka kwa ukuta wa Berlin. Alichofanya ni kujiepusha na kishawishi cha kufurahia ushindi wa vita baridi vya Marekani, kiasi cha mshangao wa kundi la waandishi wa habari wa Ikulu ya Marekani, alikataa kusafiri hadi Berlin kwa mchujo wa ushindi akijua kwamba ingewaimarisha watu wenye msimamo mkali katika Politburo na wanajeshi wanaotaka kumwondoa Mikhail Gorbachev.

Chanzo BBC

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad