Katika historia ya muziki wa bongofleva kumekua na remix nyingi ikiwemo za kimataifa, lakini sio zote zilizo fanikiwa kufanya vizuri in term of number
Sasa hizi ni remix mbili za kimataifa zilizo washirikisha wasanii wa Tanzania na kupata mafanikio makubwa zaidi kuliko original version.
YOPE Remix: wimbo uliotoka miaka miwili iliyopita kutoka kwa mwanamuziki wa Congo #innos'b ambao original version yake katika mtandao wa youtube ina takribani watazamaji million 48, lakini ukubwa zaidi wa wimbo huo ulibebwa na kushirikishwa kwa mwanamuziki @diamondplatnumz katika Remix version ambayo mpaka sasa ndio wimbo wenye watazamaji wengi zaidi katika mtandao wa youtube afrika mashariki ukiwa na zaidi ya watazamaji million 180 huku ukiwa kwenye youtube channel ya diamondplatnumz.
MANG'DAKIWE Remix: moja kati ya wimbo uliofanya vizuri sana kwa mwaka jana wa mtindo wa amapiano , kama ilivyokua kwenye YoPe Remix, miezi 6 badae @harmonize_tz aliona fursa ya kufanya Remix version ya wimbo huo tena kwa kutumia lugha ya kiswahili. Yes! iliongeza thamani na kufanywa kupendwa zaidi kiurahisi na watanzania na wale ambao hawakuekewa ugha iliyo tumika kwenye Original version, mpaka sasa wimbo huo (remix version) una watazamaji million 11' katika mtandao wa youtube ukiwa umeuzidi original version ambayo ina watazamaji million 8.
Kifupi tuseme hizi ndizo Remix za kimataifa zenye mafanikio kuliko Original version Tz🇹🇿 .