Klabu ya RS Berkane ya Morocco imewasilisha malalamiko kwa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuhusu mwamuzi wa DR Congo, Jacques Ndala Chuma alichezesha mchezo dhidi ya Simba SC na kutaka afungiwe.
Berkane wanadai Ndala alihongwa ndio maana aliwanyima penati kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Pia wanasema walipata bao la wazi lakini walinyima kwa sababu kwa sababu mchezaji wao alikuwa tayari ameshaotea (offside). Wamorocco hao walisema, Simba ilipoteza muda mwingi na mwamuzi wa akiba akaongeza dakika nne tu za kuchezwa.
Klabu hiyo inaitaka CAF kumuadhibu mwamuzi na wasaidizi wake wote kwa kufungiwa ikiwezekana kwa kushindwa kutenda haki katika mchezo huo uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.