Sababu Tano Hizi Hapa Kwanini Ukraine Imeweza Kuidhibiti Russia Mpaka Sasa



Paris, Ufaransa (AFP). Karibu wiki mbili zimepita tangu Russia ifanye uvamizi, majeshi ya Ukraine yamemudu kuwazuia wavamizi kusonga mbele, jambo ambalo limeifanya nchi hiyo isifiwe hasa na washirika wao wa Magharibi.

Wachambuzi wanasema ujasiri huo kati ya nchi yenye idadi ndogo na wanajeshi na nchi iliyo na idadi kubwa, umechangiwa na mchanganyiko wa maandalizi mazuri, mshikamano wa kitaifa na makosa ya Russia.

Hata hivyo, hali bado haieleweki kutokana na Rais Vladimir Putin kueleza kila mara kuwa hakuna kinachoweza kusimama kati yake ili kuzuia asifikie matarajio yake.

"Kimsingi, wao (Warussia) hawasongi mbele kwa kasi," amesema mwanajeshi wa cheo cha juu wa Ufaransa, aliyeomba asitajwe jina.


"Itafikia wakati fulani watalazimika kujiweka sawa upya, lakini hiyo haitamaanisha wameshindwa."

Mambo matano yanaonekana ndio yamechangia kasi ya Russia kusonga mbele katika uvamizi wake, kupungua.

Maandalizi

Ukraine, kwa msaada wa Magharibi, imeongeza uwezo wa jeshi lake kwa kiasi kikubwa baada ya mwaka 2014, wakati Russia ilipoteka rasi ya Crimea katika operesheni nyepesi na waasi wanaoiunga mkono Russia kushika sehemu ya mashariki ya nchi.


Mwaka 2016, NATO na serikali walianza programu ya mazoezi kwa ajili ya wanajeshi wa vikosi maalum vya Ukraine ambao sasa wamefikia 2,000 na ambao wameweza kusaidia raia waliojitolea.

"Waukraine wametumia miaka nane iliyopita kupanga, kufanya mazoezi, na kujipa vifaa kwa ajili ya kukabiliana na uvamizi wa Russia," amesema Douglas London, profesa mshiriki katika Chuo Kikuu cha Georgetown.

Kwa kuelewa kuwa Marekani na nchi za Umoja wa Kujihami (Nato) hazitakuja kuioko kwenye uwanja wa vita, mkakati wa Ukraine ulijikita "katika kumwaga damu Russia ili kusababisha utekaji kuwa hauwezekani," mkongwe wa Shirika la Kijasusi la marekani (CIA) aliandika.

Ujuzi wa wananchi

Russia, ikitegemea zaidi uelewa wake wa nchi hiyo tangu wakati wa dola ya Umoja wa Nchi za Kisovieti (USSR), inaonekana kuwa ilidharau majeshi ya Ukraine ya kutumia faida ya nyumbani kupambana.


Hii inajumuisha ufahamu wa uwanja wa vita wakati fulani katika mwaka njia zinageuka kuwa matope na uwezo wa wananchi kuchukua silaha wenyewe dhidi ya wavamizi.

Katika mazingira ya vita yasiyotegemewa kama hayo, majeshi dhaifu yanaweza nguvu ya ziada zilizopo dhidi ya mpinzani imara "kujua uwanja wa mapambano, ujuzi wa wananchi na mshikamano wa kijamii," amesema Spencer Meredith, profesa katika Chuo cha Usalama wa Kimataifa.

Changamoto itakuwa kubwa zaidi kama mapigano ya mjini yataibuka wakati Russia itakapokuwa inataka kujipenyeza katika majiji kama Kyiv.

"Hilo litabadili kila kitu," amesema aliye ndani ya majeshi ya Ufaransa. "Warussia wataingia matatizoni katika kila kona ya mtaa, jengo kwa jengo."


Mshikamano

Wakiongozwa na Rais Volodymyr Zelensky, ambaye amebakia Kyiv licha ya kuhatarisha maisha yake wakati Russia ikiingia maeneo ya mji huo mkuu, wananchi wa Ukraine wameonyesha uthabiti.

Wananchi wa kawaida wamejitolea kwenda mstari wa mbele, mara nyingi baada ya kuwa na uhakika kuwa familia zao zimesafirishwa kwa usalama kwenda magharibi mwa nchi au nje ya mipaka.

Picha zinazozunguka mitandaoni zimeonyesha wananchi wakitengeneza mseto wa Molotov au wakulima wakiondoa vifaa vya kijeshi vya Russia vilivyotekwa.

Ukraine haikuw ana "kingine zaidi ya kuimarisha uwezo wake wa kivita kwa kufanya mafunzo ya haraka kwa wanajeshi na matumizi ya silaha nyepesi," alisema kanali mstaafu wa jeshi nchini Ufaransa, Michel Goya.

Makosa ya kimkakati

Wachambuzi wa masuala ya kijeshi wanasema Russia ilifanya makosa ya kimkakati katika siku za mwanzo za uvamizi ambao ulianza Februari 24, ikituma wanajeshi wachache sana wa ardhini katika hatua ya kwanza ili ipate nafasi na ndege zake zipae kirahisi.


Inaonekana Russia ilitegemea kupata mafanikio ya kijeshi ndani ya siku chache.

"Kwa mipango yao walidhani wangeweza kuingiza vikosi haraka sana katika jiji la Kyiv... Lakini mapema sana wakavuja damu," alisema Michael Kofman, mratibu wa programu ya masomo ya Russia katika kituo cha Center for Naval Analyses cha Marekani.

"Hisia zao zilikuwa mbaya... unawezaje kuitaka Kyiv ndani ya siku tatu? Jeshi la Russia sasa limejipanga upya na linajaribu kufanya hilo kwa kutumia operesheni ya majeshi mchanganyiko," amesema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad