Nimeumia sana kuona Prof.Jay amerekodiwa akiwa mahututi na video hiyo kusambazwa mitandaoni. Hiki ni kiwango cha juu cha kukosa utu. Hata kama ni kutafuta pesa si kwa njia hii. Tujifunze kuheshimu utu kuliko fedha. Jiulize angekua baba yako ungemrekodi? Ikumbukwe kupiga picha hospitali bila kibali "maalumu" ni kosa kisheria.
Sera ya afya (Personal health information Protection Policy) na sheria ya mtandao (Cybercrimes Act 2015) zinalinda faragha ya mgonjwa (patient privacy and confidentiality). Kwahiyo aliyerekodi amefanya kosa KIMAADILI na KISHERIAa .
KIMAADILI amemkosea Jay, familia yake na amewakosea watanzania. Japo kosa hili halina adhabu lakini linabeba laana kwa mhusika. KISHERIA kupiga picha eneo lisiloruhudiwa na kusambaza mitandaoni ni kinyume na sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015. Adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 3 jela au faini ya TZS 5M au vyote kwa pamoja.
Lakini je nani amerekodi na kwa lengo gani? Wanaoruhusiwa kumuona Jay ni makundi matatu tu. Watoa huduma wanaomhudumia (madaktari na wauguzi), ndugu zake, na viongozi wa serikali.
Video imerekodiwa na mtu kutoka makundi hayo matatu. Hata hivyo kundi la watoa huduma linabeba asilimia kubwa zaidi kuliko makundi mengine. Si rahisi kiongozi wa serikali au ndugu yake kumrekodi. Uwezekano mkubwa upo kwa watoa huduma (madaktari na manesi) ambapo wapo nae muda mwingi.
Kwa kuwa ICU kuna CCTV, nashauri wapitie "footage" wataona ni nani aliyehusika kufanya tukio hili la kinyama. Kama ni mtumishi achukuliwe hatua za kinidhamu na za kisheria. Hatua za kinidhamu ni kama kusimamishwa kazi na kufutiwa leseni kwa kwenda kinyume na kiapo chake cha kulinda siri za mgonjwa. Na hatua za kisheria ni kupandishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kurekodi na kusambaza maudhui yasiyofaa mtandaoni, kinyume na sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015.
Akipatikana na hatia, namuomba Hakimu asimpe faini au kifungo bali amtandike vyote kwa pamoja. Atumikie miaka mitatu jela na alipe faini isiyopungua 5M kama sheria inavyoeleza. Hii itakua fundisho kwa "vishohia" wengine wanaodhani matatizo ya mtu ni fursa ya wao kuuza habari.!