Sancho, Rashford Watemwa England



MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Marcus Rashford na winga, Jadon Sancho wameachwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ambacho kitacheza michezo ya kirafiki dhidi ya Uswisi na Ivory Coast kwenye dimba la Wembley, imefahamika.

Rashford hajaitwa katika kikosi cha England tangu kumalizika kwa fainali ya Euro 2020 ambapo alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokosa penalti, huku siku za karibuni akiwa kwenye kiwango kibovu na katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumatano iliyopita ilisambaa video ikimwonyesha akiwatolea maneno machafu mashabiki.

England imeshafuzu katika mashindano ya Kombe la Dunia nchini Qatar, na wanataka kuitumia hii michezo ya kirafiki kama maandalizi na kuweka umoja kwenye kikosi chao.

Harry Maguire na Luke Shaw ni wachezaji pakee kutoka Manchester United walioitwa na Kocha, Gareth Southgate.
Kikosi kamili; Magolikipa: Jordan Pickford (Everton), Nick Pope (Burnley), Aaron Ramsdale (Arsenal).

Walinzi: Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Conor Coady (Wolves), Marc Guehi (Crystal Palace), Reece James (Chelsea), Harry Maguire (Manchester United), Tyrone Mings (Aston Villa), Luke Shaw (Manchester United), John Stones (Manchester City) na Ben White (Arsenal).

Viungo: Jude Bellingham (Borussia Dortmund), Conor Gallagher (Crystal Palace), Mason Mount (Chelsea), Jordan Henderson (Liverpool), Declan Rice (West Ham), James Ward-Prowse (Southampton).

Washanbuliaji: Tammy Abraham (AS Roma), Phil Foden (Manchester City), Jack Grealish (Manchester City), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Bukayo Saka (Arsenal), Emile Smith Rowe (Arsenal), Raheem Sterling (Manchester City).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad