Saudi Arabia yawanyonga watu 81 kwa siku moja




Saudi Arabia imesema iliwanyonga watu 81 siku ya Jumamosi - zaidi ya ilivyokuwa mwaka jana wote.

Kundi hilo - ikiwa ni pamoja na Wayemeni saba na raia mmoja wa Syria - walitiwa hatiani kwa "uhalifu mwingi wa kutisha", ikiwa ni pamoja na ugaidi, shirika la habari la serikali SPA lilisema.


 
Baadhi walishtakiwa kwa kuwa wafuasi wa kundi la Islamic State (IS), al-Qaeda au waasi wa Houthi nchini Yemen.

Mashirika ya haki yanasema kuwa wengi hawapati kesi za haki nchini Saudi Arabia, madai ambayo serikali inayakataa.

Kwa mujibu wa SPA, kundi la hivi punde lilikuwa limehukumiwa na majaji 13 na kupitia mchakato wa kimahakama wa hatua tatu.


Walishutumiwa kwa kupanga mashambulizi dhidi ya malengo muhimu ya kiuchumi, kuua au kulenga askari wa vikosi vya usalama, utekaji nyara, utesaji, ubakaji na kuingiza silaha nchini humo.

Saudi Arabia ina moja ya viwango vya juu zaidi vya wanaonyongwa duniani - ya tano katika orodha ya Amnesty International, nyingine nne zikiwa ni China, Iran, Misri na Iraq.

Iliwanyonga watu 69 mwaka jana.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad