Saudi Media Group Yatoa OFA Kuinunua Chelsea



Shirika kubwa la habari mashariki ya kati Saudi Media Group wametoa ofa ya £2.7billion ambazo ni ni sawa na dola bilioni tatu nukta tano ($3.5bn) kutaka kununua klabu inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza klabu ya Chelsea.

Klabu ya Chelsea kwa sasa wana hali ngumu ya kutaka kuhakikisha wanaweza kupata bajeti ya kutosha kutokana na serikali kuwapa ukomo wa matumizi kulingana na vikwazo waliyowekewa.

Fahamu kuwa Saudi Media Group wanakadiliwa kutengeneza kiasi cha £770million kwa mwaka wakati mnunuzi yeyote anayetokea nchini Saudi Arabia iwe kampuni ya kushirikiana au kampuni binafsi haipaswi kuwa na uhusiano wowote na serikali ya nchi hiyo.

Saudi Media Group baada ya kuweka ofa ya kununua klabu hiyo wameweka vipaumbele vyao ambavyo ni kuuboresha uwanja wa Stamford Bridge na akademi ya klabu kwenye uwanja wa mazoezi Cobham pia timu ya wanawake kuifanyia maboresho zaidi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad