Serikali yatoa Tamko Kirusi Kipya cha Corona



WAZIRI wa Afya ,Ummy Mwalimu amesema tayari ameagiza wataalamu wafuatilie kuhusu kirusi kipya cha ugonjwa wa corona kinachoitwa Omicrom.BA 1.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ummy amesema Shirika la Afya Duniani (WHO), bado linaendelea kufatili kirusi hicho, ambacho ni muunganiko wa virusi vya corona vya Delta na Omicrom, ili kujua ukali wake.

"Lakini na mimi leo nimeiambia timu yangu kufatilia, tujue kama kirusi hicho kimeingia Tanzania au bado hakijaingia, lakini kwenye nchi zingine wamethibitisha,” amesema.

Waziri Ummy amewasisitiza wananchi kupata chanjo ya corona, kwani ndio njia kuu ambayo imethibitishwa na inaweza kusaidia kupambana na maambukizi.

"Tukingalia wagonjwa waliolazwa karibu asilimia 96 hawajachanja, walioko ICU hawajachanja, lakini na vifo tunaona nao hawajachanja," alieleza Waziri Ummy.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad