Shehena ya Makombora 1,500 ya Kutungulia Ndege Aina ya Strela Yamwagwa Ukraine


Shehena ya makombora 1,500 ya kutungulia ndege aina ya Strela na bunduki 100 za MG3 zimewasili nchini Ukraine kutoka Ujerumani, Shirika la Habari la Ujerumani limewanukuu maafisa wa Serikali ya Ukraine wakisema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock alisema Jumatano kwamba vifaa zaidi vya makombora ya Strela vilikuwa vinakwenda Ukraine kufuatia kucheleweshwa kwa uwasilishaji.

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umeifanya Ujerumani kubatilisha sera yake ya kihistoria ya kutopeleka silaha katika maeneo yenye mizozo "Sisi ni mmoja wa wasambazaji wakubwa wa silaha katika hali hii, haitufanyi tujivunie lakini ni kile tunachopaswa kufanya ili kuisaidia Ukraine"

Makombora ya Strela yalikuwa katika orodha ya jeshi la zamani la Kikomunisti la Ujerumani Mashariki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad