Shirikisho la soka barani Afrika CAF imeipiga faini ya $ 108,000 klabu ya RS Berkane Kisa Simba


Shirikisho la soka barani Afrika CAF imeipiga faini ya $ 108,000 klabu ya RS Berkane ya Morocco kwa matukio mawili tofauti ya kinidhamu kwenye michezo ya hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Afrika.

1. Klabu imetozwa faini ya $ 8000 kwa kosa la mashabiki wa klabu hiyo kutupa vitu visivyotakiwa uwanjani wakati mchezo ukiendelea katika mchezo uliopigwa februari 27,2022.

2. Klabu imetozwa faini ya $ 100,000 kwa kosa la mmoja wa viongozi wake ( Majid Madrane ) kuvamia eneo la kuchezea wakati mchezo ukiendelea kwa madai ya kupinga maamuzi ya Refa.

Pia anashutumiwa kuhamasisha wachezaji wake kumvamia Refa kupinga maamuzi kwenye mchezo huo jambo ambalo lilipelekea mchezo kusimama kwa dakika tano kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam Simba akiibuka na ushindi wa bao 1-0.

Hivyo Majid Madrane amefungiwa kutojihusisha na soka kwa muda wa miezi 12.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad