Mabingwa watetezi wa ligi kuu bara, Simba SC wameendeleza moto wao pale walipoishia baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Dodoma jiji.
Magoli ya Simba yamefungwa na Clautos Chama kwa mkwaju wa penati dakika ya 57, huku Meddie Kagere akiweka chuma ya pili dakika ya 75.
Simba sasa anafikiaha pointi 37 baada ya michezo 17.