Staa wa filamu za Kinigeria " Baada ya Miaka Mitano Nitakufa"


Staa wa filamu za Kinigeria wa Nollywood nchini Nigeria, Kemi Afolabi, ameweka wazi kwamba madaktari wake wqalishamwambia anahudumia miaka mitano tu katika uhai wake kabla ya kupatana na umauti kutokana na kwamba ugonjwa anaougua hauna tiba rasmi.

Afolabi alisema kwamba katika miaka hiyo mitano ya kutumikia maisha, tayari ameshaumega mwaka mmoja na sasa amebaki na miaka minne zaidi kabla ya Malaika Izraili mtoa roho kufanya kazi yake.


Nguli huyo wa kuigiza filamu za Naijeria ana umri wa miaka 43 na alisema taarifa hizo alizipokea kama Hezekiah kwenye biblia aliyeambiwa ana miaka 15 ya kuishi kwenye ulingo wa dunia. Alisema madaktari walimuambia anaugua ugonjwa wa Lupus ambao aghalabu hutokea kinga ya mwili inaposhambulia viungo mwilini kupelekea mwili kupoteza uwezo wa kujikinga kutoka kwa magonjwa mbalimbali. Ugonjwa huo hauna tiba zaidi ya kifo tu!

Akizungumza na mwanahabari Chude Jideonwo katika mahojiano ya kipekee, Afolabi alibubujikwa na machozi alipofichua kwamba alishaambiwa ana miaka 5 tu ya kuishi hata baada ya kugharimika pakubwa kifedha kujaribu kutafuta tiba ya ugonjwa huo ambayo hadi sasa hajaipata.

“Nina ugonjwa wa lupus. Haitibiki. Inabidi utumie dawa maisha yako yote. Nimetumia zaidi ya Naira milioni 1 kwa matibabu, lakini sikupata matokeo niliyotaka.” Alisema Afolabi.

Muigizaji huyo akiwa katika hamaki na majonzi mengi alisema kwamba daktari wake alimuambia muda wote ahakikishe ako karibu na wapendwa wake kwa muda huu aliosalia nao wa maisha yake.

“Hakikisha uko pamoja na wapendwa wako. Angalau, bado una hadi miaka mitano.” Afolabi alimnukuu daktari wake.

Mapema mwezi Januari, mwaka huu Afolabi aliposti kwenye ukurasa wake wa Instagram na kutangaza kwamba amegundulika kuwa na ugonjwa usiotibika ambao baadae aliweka wazi kuwa ni Lupus.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad