Reposted from @stevenyerere2 Haya Maana naona Simu kama 100000 zinaingia wacha Niseme,.....Kwanza Kabisa nimeona Mkeka uliotoka Wa Tuzo za BASATA , Niwapongeze sana BASATA kwa Ubunifu wa Tuzo hizo Hakika Ni muda sana Wasanii wa Mziki walikuwa na hamu ya Tuzo maana Tuzo Huongeza juhudi Maarifa Ubunifu na jitihada pia.,
Ndugu zangu Viongozi wangu wa BASATA nia ya Tuzo ni Kuheshimu kazi nzuri walizo fanya Wasanii wetu kwa kipindi chote,... lakini kikubwa Zaidi Tuzo hutuunganisha watu wetu wote kuwa kitu kimoja,..
Kutoa maoni kwa Ajiri ya kuboresha sio dhambi..
Chombo chochote kile kinacho ongoza watu lazima kiwe kinakubali kukosolewa kwa nia ya kujenga na sio kila anayekosoa basi hawatakii Mema apana Yawezekana ndio anawafumbua macho ili muweze kukaa chini na kupata kitu kizuri zaidi.,.,..,
Ndugu zangu BASATA kuna haja mkaa chini tena mkajitafakari kwa hili Maana naimani vinaongeleka kwa maslahi ya Mziki wetu na mashabiki wa Mziki Tanzania 🇹🇿.
Leo hii wapo Watanzania wanataka kuona Zuchu kashindanishwa na nani, Leo hii Watanzania wanataka kuona MBOSO yupo kundi gani Ray yupo kwenye kategoli ipi lakini hili mnataka kulifumbia macho kwa Jeuli tu haiwezekani.,,
Tuzo ndio sehemu pekee ambayo haina makundi kuna mziki mzuri sio Matimu flani no hapa ni Mziki tu., Na tunapo sema Tuzo za ndani hakuna mtu atazipinga maana heshima huanzia nyumbani kwako kwanza.,.,.,
Naimani Sana na Mh Mchengelwa kwa hili naimani naye kubwa atatumia Busara kukaa kitako na @wasafi pamoja na uongozi mzima kwa Faida ya mashabiki wa mziki wetu.,.,.,
Kama kweli Tuna nia ya kuboresha sanaa yetu basi hakuna haja ya kuvutana kuna haja ya kukaa chini na kukubaliana na WASANIII wote kuwa tunaenda kujenga nyumba 1 haina haja ya kugombea Fito.,.,.,
Niombee Wizara yetu pendwa tuangalie mchakato huu upya kabisa kwa maslahi ya kuinua na kupeleka mbali zaidi mziki wetu.,.,.,.,