Taifa Stars yaichapa Afrika ya Kati



TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenye mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliomalizika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katika mchezo huo ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Stars kwenda mapumziko ikiongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Novatus Dismas dakika ya kumi kwa mpira wa adhabu.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko kwa Stars kuwaingiza Simon Msuva, Lusajo Mwaikenda, Farid Mussa na Joshua Mwakasaba kuchukua nafasi za Abdillahie Yussuph, Haji Mnoga, Ben Starkie na Nickson Kibabage.

Kwa upande wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alitoka Toropite Tresor na kuingia Fourmy Chistopher aliyeingia kuongeza nguvu eneo la ulinzi.


 
Mabadiliko hayo yalionesha kuinufaisha zaidi Stars ambayo ilishambulia kwa kasi mara kwa mara lango la Afrika ya kati lakini hadi kufika dakika ya 60 ya mchezo matokeo yalikuwa 1-0.

Afrika ya kati ilifanya mabadiliko mengine dakika ya 62 kwa kuwatoa Dembakizi Sidney na Dimokoyen Saint Fort na kuingia Gaopandia Jospin na Yawanendji Theodore lakini dakika moja baadae Stars ilipata bao la pili kupitia kwa Mbwana Samatta.

Samatta alifunga bao hilo kwa kumalizia pasi safi ya Farid Mussa lakini dakika ya 66 Afrika ya Kati ilipata Mkwaju wa Penalti baada ya nyota wake aliyeingia akitokea nje Yawanendji kuchezewa madhambi nani ya boksi la 18 la Stars.


Mkwaju huo wa Penalti ulipigwa na huyo huyo Yawanendji na kuzama moja kwa moja ukimshinda kipa Metacha Mnata na ubao wa matokeo kusomeka 2-1.

Dakika 73, Stars ililazimika kufanya mabadiliko baada ya mfungaji wa bao la kwanza, Novatus kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Aziz Andambile na dakika sita baadae Afrika ya kati walijibu mapigo kwa kumtoa Ban Thibaut na kuingia Ngam-Ngam Saint.

Dakika ya 86 Stars alitoka Kelvin John na kuingia George Mpole kwa huku kwa Aftika ya kati Pirioua brad na Saint Fort wakitoka na nafasi zao kuchukuliwa na Mvondeze Geprge na Dotte Bisafi.

Dakika ya 90 ya mchezo mshambuliaji George Mpole aliifungia bao la tatu na la mwisho Stars na kufanya mechi kumalizika kwa matokeo ya Stars 3-1 Afrika ya kati.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad