Mabingwa wa Tanzania Simba Sc wameshika nafasi ya 98 kwa ubora wa vilabu duniani ikiwa na alama 137.5
Taarifa hii ni Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2021 ya shirika la IFFSH (linalotambuliwa na FIFA), shirika ambalo limekuwa likifanya tafiti na tathimini za masuala mbalimbali ya soka Duniani
Simba SC imeshika nafasi ya 98 kidunia kwa ubora wa vilabu ikiwa na alama 137.5 wakifungana na Rijeka ya Croatia.
Katika Mwaka 2020 Simba walikuwa nafasi ya 361 na sasa wamepanda hadi 98 katika ripoti ya shirika hilo
Katika Ripoti hiyo Klabu inayoongoza ni SE Palmeiras ya Brazil na Club Atletico Mineiro ya Brazil pia
Nafasi ya Tatu inashikwa na Manchester City na nafasi ya nne ni Chelsea zote za England
Cc @exaud_msaka_habari✍
#DizzimTv #DizzimUpdates #DizzimSports