🍁Juma Nature aliingia kwenye muziki akaukuta umejaa umarekani mwingi na akabadilisha mchezo kabisa. Silaha yake kubwa ilikuwa ni storytelling.
🍁Ipo wazi Juma Nature ndio bingwa wa storytelling kibongobongo. Alianza na story ya kigheto ghetto mpaka simulizi za ex wake Sinta. Na alivutia kwa sababu alitumia ucheshi na lugha za uswazi.
🍁Kwa sasa muziki wa bongo unafanya vizuri kwenye waimbaji ila upande wa rap ni kama umekufa. Kwa sasa hawezi simama rapa akachana nchi ikastuka.
🍁Shida kubwa marapa wa sasa wamewekeza kwenye mistari konde yani ufundi wa kugeuza geuza mashairi na wengine wameingia kwenye trap wanajikuta kina Dababy au Migos hakuna localisation.
🍁Ma-MCs wadogo jifunzeni kwa Juma Nature aliingia kwenye game na silaha yake kubwa ilikuwa kuelezea story haswa za uswazi. Aliisimamisha mitaa akawa jina la mchezo.
🍁Jifunzeni storytelling... hakuna mwanadamu anayeweza kuukwepa mtego wa story kila binadamu anapenda kusikia visa mbalimbali.
🍁FA alitupa kisa cha aliyekufa kwa ngoma... Profesa akatuletea mwanasiasa muongo muongo kwenye ndio mzee... Ngwea akatupa story za ghetto lake.... J Mo akatupa mawili matatu kuhusu mabalaa ya mvua na jua...Nature ndio aliua kabisa akatusimulia Mzee wa Busara, Drama za Sinta. Mtoto Iddi nk
🍁Hii ndio siri pekee nataka niwape vijana wadogo mnaoingia kwenye muziki wa hiphop kama mnataka kutengeneza pesa...Hakikisha unachokiandika hata yule beki tatu anaeosha vyombo nyumbani anaweza kuvutiwa na kukiimba.
👉Maisha ya binadamu ni hadithi.
👉Lakini msiandike story kama mtu anasoma kitabu cha Shigongo. Andaeni content zenye ubunifu wa kimuziki. Hii ndio siri ya Juma Nature kuubadili mchezo na akaibeba Temeke mabegani, Storytelling.
NB: Akitokea storyteller wa rap kuna pesa yake nyingi sana ya kubadilisha maisha yake na family yake.
msumbufu_