Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria sasa anadai kuwa Rais Uhuru Kenyatta anataka kuwa Waziri Mkuu katika serikali ya kiongozi wa ODM Raila Odinga
Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria sasa anadai kuwa Rais Uhuru Kenyatta anataka kuwa Waziri Mkuu katika serikali ya kiongozi wa ODM Raila Odinga
Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria sasa anadai kuwa Rais Uhuru Kenyatta anataka kuwa Waziri Mkuu katika serikali ya kiongozi wa ODM Raila Odinga.
Katika taarifa ya Jumatatu, Kuria alisisitiza kuwa Rais anapanga kutostaafu.
Hata hivyo, alionya kwamba hawataruhusu hilo kutokea.
"Ukweli ambao hata yeye anajua ni kwamba anataka muhula wa tatu- Wakati huu kama Waziri Mkuu katika serikali ya Baba. Hili ni jambo lisilopendeza na halikubaliki kwetu wana na mabinti. ya wakulima wa Kikuyu. Tutapinga!" Alisema kwenye ukurasa wakewa Facebook.
Hili ndilo shambulio la hivi punde kati ya mashambulio mengi ya mbunge huyo dhidi ya Rais Uhuru.
Mnamo Ijumaa, Machi 18, Kuria alionya Rais akisema alihatarisha kulaaniwa kwa kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani kwa urais.
Akizungumza mjini Kiambu akiandamana na DP Ruto kwa misururu ya mikutano eneo hilo, Kuria alisema rais atalaaniwa kwa kukaidi kiapo kilichotolewa na jamii.