Ujerumani Yagoma Kutuma Ndege za Kivita Ukraine



Ujerumani imesema haitatuma ndege za kivita nchini Ukraine, baada ya Marekani kukataa pendekezo la Poland la kuhamisha ndege zake za kivita aina ya MiG-29 nchini Ukraine kupitia kambi ya Marekani nchini Ujerumani.

Kansela Olaf Scholz anasema Ujerumani “imetoa kila aina ya vifaa vya ulinzi” ikiwa ni pamoja na silaha, lakini anasema “bila shaka ndege za kivita sio sehemu ya hilo”.

Wakati huo huo nchini Uingereza, Serikali inasema “haiwezekani” kwa marubani wa Nato na ndege zake kuzishambulia ndege za Urusi.

Msemaji wa Waziri Mkuu anasema Boris Johnson “amesema mara kwa mara” kuwa amejitolea “kutoa silaha ambazo Ukraine inahitaji”.


 
Mapema, Uingereza ilisema inaongeza usambazaji wake wa silaha kwa Ukraine, ikituma makombora 1,615 zaidi ya kupambana na vifaru na makombora ya Masafa marefu ya Javelin.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad