Ukraine Yasema Urusi inatega Mabomu Katika Bahari Nyeusi

 


Ukraine imeituhumu Urusi leo kwa kutega mabomu katika Bahari Nyeusi. Imesema baadhi ya mabomu hayo yameteguliwa katika pwani ya Uturuki na Romania wakati kitisho kikiendelea kuongezeka kwa meli za kusafirisha bidhaa katika kanda hiyo. 

Bahari Nyeusi ni njia muhimu ya kusafirisha nafaka, mafuta na bidhaa za mafuta. Bahari hiyo inatumiwa na Bulgaria, Romania, Georgia na Uturuki pamoja na Ukraine na Urusi. 


Katika siku za karibuni timu za kijeshi za Romania na Uturuki zimehusika katika kutegua mabomu ya kuelea majini yaliyopatikana katika mipaka yao ya baharini. 


Wizara ya Mambo ya kigeni ya Ukraine imesema Urusi inatumia mabomu ya jeshi la wanamaji ambayo yanaelea kama silaha inayotishia safari za meli na maisha ya watu baharini.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad