Umoja wa Ulaya (EU) umetoa tamko la kuendelea kulaani kitendo cha Urusi kuivamia #Ukraine na kushawishi Mataifa mbalimbali zikiwemo Nchi za Afrika kujitokeza hadharani kuipinga Urusi
Tamko hilo limetolewa na baadhi ya Mabalozi wa Nchi za Ulaya waliopo #Tanzania ambao Nchi zao ni Wanachama wa EU, wakieleza kuungana huko hakutakuwa na maana Urusi itasitisha uvamizi muda huohuo lakini itakuwa na maana kubwa kwa kuionesha Urusi jinsi Dunia ambavyo haikubaliani naye
Walioshiriki kutoa tamko hilo Machi 22, 2022 Jijini Dar es Salaam ni mabalozi wa Ufaransa, Ujerumani, Poland, Uholanzi, Sweden, Finland, Hispania, Italia na Balozi wa EU