Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi inasema jeshi la Urusi linaendelea na mashambulizi yake kwa urahisi katika uwanja mapambano huko nchini Ukraine.
Msemaji wa wizara hiyo, Igor Konashenkov anasema kwa sasa vikosi vinakaribia mji mkuu Kiev, kituo cha anga cha Vasylkiv na kadhalika wamekidhibiti kituo cha ujasusi wa kijeshi cha Ukraine cha Brovary.
Kwa mujibu wa Urusi, vikosi vyake kwa ushirikiano wa vikosi vya wanaotaka kujitenga kutoka Luhansk na Donetsk wamethibiti maeneo mengi kwa upande wa mashariki mwa Ukraine.
Mwanzoni mwa vita Februari 24, wanaotaka kujitenga walikuwa wakidhibiti asilimia 30 ya maeneo hayo. Lakini kwa sasa kwa mujibu wa takwimu za Ukriane asilimia 70 ya jimbo la Luhansk lipo katika udhibiti wao