Urusi Yakiri Kutumia Kombora Hatari la Hypersonic



Waziri wa Ulinzi wa Urusi amethibitisha kuwa nchi yake imetumia bomu hatari la hypersonic kwa mara ya kwanza kulishambulia na kuliteketeza ghala la silaha nchini Ukraine.

Bomu aina ya Hypersonic lina uwezo wa kusafiri kwa umbali wa kilomita 4,900 kwa saa na kuongeza kasi hadi kufikia kilomita 12,350 kwa saa, likiwa pia na uwezo wa kubeba kichwa cha mzinga wa nyuklia chenye uzito wa kilo 480 ambayo ni mara 33 ya bomu lililoshushwa na Marekani katika ardhi ya Hiroshima na Nagasaki nchini Japan wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.

Putin amelielezea bomu hilo kama silaha muhimu kwenye mapigano na kuinadi kuwa inaweza kusafiri mara kumi zaidi ya spidi ya sauti na kwamba hakuna nchi ya Magharibi hata moja yenye teknolojia ya kuzuia bomu hilo kupitia mfumo wa usalama wa anga.

Bomu hilo lina uwezo wa kusafiri umbali wa kilometa takribani 2011 huku likiwa na uwezo wa kusababisha madhara makubwa mahali litakapotua ambapo kwa miaka mingi, Urusi imekuwa ikipinga matumizi ya silaha za masafa marefu aina ya hypersonic.


 
Meja Jenerali wa jeshi la Urusi, Igo Konashenkov amesema licha ya bomu hilo, Urusi pia ilitumia makombora kusambaratisha ngome ya majeshi ya Ukraine iliyopo karibu na bandari ya bahari nyeusi ya Odesa.

Naye msemaji wa vikosi vya anga vya majeshi ya Ukraine Yuri Ignat amethibitisha kuwa ni kweli ngome yao imeshambuliwa lakini hakuwa na taarifa ni aina gani ya makombora yalitumika kushambulia eneo hilo.

Ignat alinukuliwa akisema:
“Maadui walilenga ngome yetu lakini hatuna taarifa ni aina gani ya makombora wanayotumia, kuna madhara, uharibifu na uteketeaji wa silaha, wanatumia makombora yote yaliyomo kwenye ghala lao la silaha.”

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ameionya Urusi kuendelea na mashambulizi ndani ya nchi yake na kusema utekelezaji wa mashambulizi hayo ni dhambi ambayo itarithishwa kwa vizazi na vizazi kwa wananchi wa Urusi.

Kwa upande mwingine, mshauri wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Ukraine, Vadym Denyshenko ameilaumu serikali ya Belarus kwa kutoa huduma za upasuaji kwa wanajeshi wa Urusi walioumia kwenye mashambulizi dhidi ya vikosi vya Ukraine.

Denyshenko amenukuliwa akisema:
“Vituo vya afya vyote nchini Belarus vyenye idara za upasuaji vimejaa wanajeshi wa Urusi, inafikia muda hadi raia wa Belarus wenye kuhitaji huduma ya upasuaji wanasitishiwa ratiba zao au kuondolewa kwenye raiba kabisa ili tu wanajeshi wa Urusi wapatiwe huduma, idadi kubwa ya vifo inarekodiwa kwa wanajeshi wengi wa Urusi wanaofariki kutokana na kujeruhiwa vibaya.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad