Urusi yaonya Marekani: Tutawararua na kuwaweka katika nafasi yenu, msitujaribu!


Urusi inaituhumu Marekani kwa kuendeleza njama ya kuisambaratisha kwa kuchochea ulimwengu dhidi yake, utawala wa Moscow ukisema hilo halitawezekana
Onyo la Urusi linajiri siku mbili tu baada ya taifa hilo kumpiga marufuku Rais wa Marekani Joe Biden kukanyaga nchini humo
Urusi imeonya Marekani kuwa ina uwezo wa kuirarua Marekani kwa vipande na kuiweka katika nafasi yake, utawala wa Moscow ukiituhumu serikali ya Jose Biden kwa kuendeleza mipango ya kuisambaratisha Urusi.

Urusi Yaionya Marekani dhidi ya Kuendelea Kuichokoza: "Msitujaribu, Tutawararuararua kwa Vipande"
Rais wa Marekeni Joe Biden (kushoto) na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin.
Dmitry Medvedev ambaye alihudumu kama rais wa Urusi kati ya 2008 na 2012 na ambaye kwa sasa ni Katibu wa Baraza la Usalama la Urusi alisema kuwa Marekani ilikuwa na njama ya kuuchochea ulimwengu dhidi ya Urusi ili kushurutisha taifa hilo kupiga magoti.

“Haitafaulu. Urusi ina nguvu za kuwaeka maadui wetu katika eneo lao,” Medvedev alisema.

Tangu kuvamia Ukraine mnamo February 24, Marekani na maswahiba wake wa bara Ulaya na Asia, wamewaekea vikwazo viongozi wa Urusi, kampuni za Urusi, wanabiashara wa taifa hilo na kuitenga Urusi kwenye uchumi wa dunia.


 
Msitulaumu: Urusi Yasema Vikwazo vya Marekani Kulaumiwa kwa Gharama Kubwa ya Maisha Kenya
Rais Vladimir Putin anasema kuwa kile anachoita ‘oparesheni spesheli nchini Ukraine’ kilihitajika kwa sababu Marekani ilikuwa ikiitumia Ukraine kuitishia Urusi na Urusi haikuwa na budi ila kulinda raia wake dhidi ya kuangamizwa na Ukraine.

Onyo hili linajiri siku mbili tu baada ya taifa hilo kumpiga marufuku Rais wa Marekani Joe Biden kukanyaga nchini humo pamoja na aliyekuwa Katibu wa Serikali ya Marakeni Hillary Clinton pamoja na mwanawe Biden, Hunter.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la CBS News, Urusi vilevile itafungia mali za wale wote waliotajwa katika orodha hiyo.

Marekani ilijiunga na jamii ya kimataifa kwa kutelekeza vikazo dhidi ya Urusi kufuatia hatua yake ya kuvamia taifa jirani la Ukraine.

Kando na vikwazo hivyo, kampuni nyingi za Kimerekani zimekoma kufanya biashara katika taifa la Urusi.

Urusi nayo imeshikilia kuwa inapanga kuweka vikwazo zaidi katika siku za usoni, vikwazo hivi vikilenga wafanyabiashara na watu katika vyombo ya habari.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad