Wizara ya ulinzi ya Ukraine imechapisha ripoti yake ya kila siku kuhusu mzozo huo. Haya hapa mambo muhimu:
Vikosi vya Urusi vimepoteza ndege na helikopta 88 tangu vita kuanza
Marubani kadhaa wa Urusi wamekamatwa.
Wanajeshi wa Ukraine wanaendelea kuulinda mji wa bandari wa Mariupol kusini-mashariki.
“Kiasi kikubwa” cha vifaa vya Urusi vilikamatwa katika mkoa wa Mykolaiv – kusini, karibu na Odesa.
Wanajeshi wa Urusi “wamevunjwa moyo” na nguvu ya upinzani Waukraine
BBC haijafanikiwa kuthibitisha madai ya wanajeshi wa Ukraine wanadai. Urusi imetoa maelezo machache ya hasara iliyopatwa vikosi vyake nchini Ukraine lakini wataalam wa kijeshi wanatathmini kwamba imeshangazwa na nguvu ya upinzani wa Ukraine na imekumbwa changamoto ya kupata njia za usambazaji bidhaa na ari ya askari.