“NINGEKUWA na uwezo ningehama Urusi sasa hivi. Ningefanya hivyo. Lakini siwezi kuacha kazi yangu,” anasema Andrey.
Hataweza kumudu mpango wa kununua nyumba kwa mkopo wa malipo ya pole pole huko Moscow baaada ya viwango vya riba kuongezwa.
Mamilioni ya raia wa Urusi kama yeye, wameanza kuhisi athari za vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na nchi za Magharibi, kuiadhibu nchi hiyo kutokana na hatua yake ya kuvamia taifa jirani la Ukraine.
“Napanga kutafuta wateja wapya nje ya nchi haraka iwezekanavyo na kuhama Urusi kwa pesa nilizokuwa nikihifadhi kwa awamu ya kwanza,” anasema mbunifu huyo wa viwanda mwenye umri wa miaka 31.
Anaongeza: “Naogopa kuwa hapa watu wamekamatwa kwa kuongea dhidi ya ‘msimamo wa chama.’ Naona aibu na hata sikuwapigia kura walio madarakani.”
Vikwazo vya sasa vinavyoikumba Urusi vinaelezewa kuwa vita vya kiuchumi vinalenga kuitenga nchi hiyo na kusababisha mdororo mkubwa wa uchumi.
Viongozi wa Magharibi wanaamini hatua ambazo hazijawahi kushuhudiwa zitaleta mabadiliko katika fikra huko Kremlin. Warusi wa kawaida wanakabiliwa na kuona akiba yao ikifutwa. Maisha yao tayari yanavurugika.
Vikwazo dhidi ya baadhi ya benki za Urusi ni pamoja na kuzikata kwenye Visa na Mastercard na hivyo basi Apple Pay na Google Pay.
Daria, 35, meneja wa mradi huko Moscow, alisema hii inamaanisha hangeweza kutumia Metro. “Huwa nalipa kupitia simu yangu lakini haikufanya kazi. Kuna baadhi ya watu waliokabiliwa na tatizo hilo,” ameeleza.
Ilibainika kuwa vizuizi hivyo vinaendeshwa na benki ya VTB ambayo iko chini ya vikwazo na haiwezi kukubali Google Pay na Apple Pay.
Anasema, “ilinibidi kununua kadi ya metro badala kama njia mbadala,” na kueleza kuwa “sikuweza pia kulipa katika duka leo kwa sababu hiyo hiyo.”
Kufanya malipo ya usafari kwenye treni ya mwendo kasi na ununuzi katika maduka sasa ni vigumu zaidi kwa Warusi.
Jumatatu iliyopita siku tatu baada ya Rais Putin kuivamia Ukraine na siku mbili baada ya mataifa ya Magharibi kutangaza vikwazo dhidi yake Urusi iliongeza maradufu kiwango chake cha riba hadi asilimia 20 katika juhudi za kukabiliana na vikwazo baada ya thamani ya sarafu yake kushuka kwa viwango vya juu.
Soko la hisa bado limefungwa huku kukiwa na hofu ya kuuzwa kwa hisa nyingi. Kremlin inasema ina rasilimali za kutosha kukabiliana na vikwazo, lakini hilo linatiliwa shaka. Mwishoni mwa wiki, watu walihangaika mabenki kutokana na hofu iliyowafanya kukimbilia kutoa fedha.
“Hakuna sarafu ya dola, wala roubles hakuna kitu! Hata kama hakuna roubles sio hoja kwasababu sina haja nazo,” alisema Anton (jina limemadilishwa), ambaye yuko na umri ya miaka na ambaye alikuwa anapiga foleni katika mashine za ATM mjini Moscow.
“Sijui kitakachotokea baadaye. Nahofia huenda tukakabiliwa na hali ya Korea Kaskazini na Iran,” anaeleza.
Kununua sarafu za kigeni kunaigharimu Urusi karibu asilimia 50 zaidi ya ilivyokuwa wiki moja iliyopita ikiwa zitapatikana.
Mwanzoni mwa mwaka 2022 dola moja iliuzwa kwa karibu roubles 75 na euro kwa 80. Lakini vita hivi vipya vimeweka rekodi mpya – wakati mmoja siku ya Jumatatu dola moja iligarimu roubles 113 na euro moja kwa roubles 127.
Rouble v dollar
Kwa Warusi, kiwango cha dola dhidi ya ruble imekuwa suala nyeti kwa muda mrefu. Katika miaka ya 1990 kufuatia kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti, dola ilikuwa sarafu pekee imara ambayo Warusi walitumia kuweka akiba yao – dau salama zaidi lilikuwa chini ya godoro.
Wakati Serikali ya Rais Boris Yeltsin iliposhindwa kulipa deni lake mwaka 1998, wale ambao walikuwa wakilala na pesa za chini ya godoro walihisi kuwa salama.
Hata hivyo, katika muongo uliofuata hatua mbalimbali za benki kuu zilisaidia kuwahakikishia Warusi kuhusu ruble.
Amana zilizowekwa katika sarafu ya Kirusi zilianza kukua na ndivyo pia kiasi cha fedha ambacho Warusi waliwekeza katika hisa za makampuni ya Kirusi.
Lakini wakati wowote kunapotokea hali ya kutokuwa na uhakika, Warusi hukimbilia mashine ya ATM iliyo karibu ili kutoa dola.
Watu wanasimama kwenye foleni nje ya taasisi ya mikopo ya Urusi ya Sberbank huko Moscow, Urusi, wakati hali haikuwa hivyo.
Mara tu vita vilipoanzishwa nchini Ukraini wiki iliyopita, Warusi walimiminika kwenye vituo vya fedha, kutokana na funzo walilopata katika katika mizozo ya awali.
Ilya (jina limebadilishwa), ambaye yuko katika miaka yake 30, amemaliza tu kulipa deni la kununua nyumba kwa mkopo huko Moscow. Anasema hawezi kuhama “wakati wowote hivi karibuni.”
“Wakati operesheni ya Donbas ilipoanza nilienda kwa ATM na kutoa akiba niliyokuwa nayo Sberbank kwa dola. Sasa ninaiweka chini ya mto wangu.
“Akiba yangu iliyobaki bado iko kwenye benki: nusu kwa dola na iliyobaki kwa sarafu ya rubles. Mambo yakizidi kuwa mabaya, nitazitoa zote. Naogopa kwa sababu natarajia kutokea kwawimbi la wizi. Lakini hali ndivyo ilivyo,” ameeleza.
Picha kwenye mitandao ya kijamii zimeonesha milolongo mirefu kwenye mashine za ATM na maeneo yaubadilishanaji wa fedha kote nchini katika siku za hivi karibuni, huku watu wakiwa na wasiwasi kwamba kadi zao za benki zinaweza kuacha kufanya kazi au kwamba kikomo kitawekwa kwa kiasi cha pesa wanachoweza kutoa.
Dola na euro zilianza kuisha ndani ya saa chache baada ya uvamizi huo. Tangu wakati huo, kiasi kidogo sana cha sarafu hizo zimepatikana na kuna kiwango cha juu cha rubles ngapi unaweza kutondoa.
Watu wakiwa kwenye foleni ya mashine ya kutoa pesa ya ATM huko St Petersburg siku ya Jumapili.
Akiwa amesimama katika moja wapo wa foleni mjini Moscow, Evgeny (jina limebadilishwa), 45, alisema anataka kutoa pesa zake zote alipe mkopo wa nyumba alioyonunua.
“Kila mmoja ninayemjua anawasiwasi. Kila mtu ana msongo wa mawazo. Sina shaka hali itakuwa mbaya zaidi. Vita ni mbaya War.”
“Nadhani ‘nchi kubwa’ zinapima nguvu za kila mmoja, kuamua ni ipi iliyo na uwezo. Na kila mtu anateseka.”
Marat (35), alisema: “Leo ni siku ya kwanza niliamua kutoa pesa, na sikupata shida yoyote. Nilitoa rubles zilizokuwa tu.
“Mimi sio mzuri wa kutabiri yatakyofanyika isku zijazo lakini nashuku maisha yetu yakuwa magumu sana. Wacha tusubiri.”
Ni rahisi kupata Roubles kuliko dola lakini iliwa na thamani ya chini kuliku ilivyokuwa awali. Tatizo la pesa taslimu haliko Moscow pekee: watu wamekuwa wakikimbia kuzunguka Perm, Kostroma, Belgorod na miji mingine ya mkoa ili kupata dola au euro, BBC Idhaa ya Kirusi inaripoti.