Katika siku ya kumi na sita ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, jeshi la Urusi limepanua mashambulizi yake hadi mji mwingine mkubwa, Dnipro, na kuendeleza mashambulizi yake ya mabomu ambayo yameharibu nyumba na miundombinu, hasa katika mji wa Mariupol ambako hali ni mbaya, kwa hatari ya kuchukuliwa "vikwazo vingine vikali" kutoka nchi za Magharibi. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakukutana Ijumaa hii kwa ombi la Moscow.
Pointi kuu:
► Urusi inaajiri "wauaji kutoka Syria" ili "kuharibu" Ukraine, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameshutumu Ijumaa hii, baada ya Moscow kubaini kwamba iko tayari kutuma mamluki wa Syria kupigana kwa upande wa vikosi vya Urusi nchini humo.
► Kwenye uwanja wa vita, vikosi vya Urusi viko kwenye lango la mji mkuu Kiev wakati miji ya Mariupol, Kharkiv na Mykolaiv - hatua ya mwisho kabla ya bandari ya Odessa - inakabiliwa na mashambulizi ya majeshi ya Urus. Hali ni mbaya hasa huko Mariupol, ambapo hospitali ya watoto ilikumbwa na mashambulizi ya anga siku ya Jumatano, na kuua watu watatu, akiwemo msichana mdogo.
► Mashambulizi matatu ya anga yamelenga miundombinu ya kiraia huko Dnipro Ijumaa asubuhi. Ndege za Urusi pia zimeshambulia viwanja viwili vya ndege vya kijeshi huko Lutsk na Ivano-Frankivsk.
► Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana Ijumaa hii, kwa ombi la Moscow.
► Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Ulaya wanakutana Versailles kutafakari njia za kupunguza utegemezi wao kwa gesi na mafuta ya Urusi.
► Takriban watu 100,000 walihamishwa katika kipindi cha siku mbili kutoka miji ya Ukraine, alitangaza rais wa Ukraine, ambaye pia analishutumu jeshi la Urusi kwa kuzuia uhamishaji wa raia kutoka miji iliyozingirwa ya Mariupol na Volnovakha na kufanya shambulio kwenye maeneo salama ya kiutu.
► Kwa kukabiliana na vikwazo vya nchi za Magharibi, mamlaka ya Urusi imetangaza vikwazo hadi mwisho wa mwaka kwa mauzo ya nje katika sekta za kilimo cha matibabu, pamoja na teknolojia, mawasiliano ya simu na vifaa vya umeme.